Toka kwa: Ukoo Flani Mau Mau ft Kamah, Winyo & Kitu Sewer
Nyimbo: Angalia Saa
Producer: Eric Musyoka "Musyoks"
Muunda mdundo: Eric Musyoka "Musyoks"
Studio: Decimal Records
Tarehe iliyo toka: 2008
[Verse 1: Kamah]
Damu jasho machozi/
Mau Mau ikashinda war mashabik wakaenda na trophy/
Matigari hana ata ka-ploti/
Serikali inataka imfukuze Nairobi/
Mangaa wanataka wamangishe G-Rongi/
Hawana kodi/
They don know who we be haikosi/
White highlands no more/
Si siri hawatoshi/
Hii vita imepita rangi ya ngozi/
Na kabila najua ni mbili tu/
Maskini na mdosi/
So synchronising time 205/
Decolonizing minds/
Msisemi mliji-hypnotise/
Wana-run divisions za sheke wa kifiro/
Bugi mato/
Mtu anatusi matiti ya mother alinyonya/
Alafu anapigiwa makofi na kilo/
Wa-shoot Muthoni wa Nyanjiru/
The same route wa-rape mama yetu Njeri/
Hii si ni betrayal ya ma-hero/
Ka Kenya ni matrix nani ndio Neo/
Ka Kimathi hakuwa the one/
Then society iko drunk na opium/
Ilivyosemekana na Karl Marx/
Na philanthropic church/
Na-pay tax kuwa harassed daily/
Mothers can't even protect their babies/
Wanaume hawaezi protect ma-ladies/
Wao haki iwe ngao/
Vita vya bunduki skia mikuki/
Bullets ivuke nayo/
Tangu era za nyayo/
Wanakumanga msee/
[Verse 2: Kitu Sewer]
Tukiwapasulia pazia tu-expose/
Zile ghasia nyi hufanya/
Mtatukuta kwetu mtatuvamia/
Hiyo ilikuwa last year/
Nilidhani mtaadisia sense/
Kwa wimbo zenu tulisinzia/
Bado mnasinzia this year/
Unaeza teta ukishukiwa kimakosa/
Unaeza tema ukishibishwa uongee mbaya/
Unaeza hepa ukinusiwa/
Unaeza tema ukizidiwa/
Hakuna haja ya kuji-force kitu hautaki/
Si unajua vile kwao huenda/
Mgema akisifiwa/
Writer m-famous aliibiwa/
Na wife yake aka-rape-iwa na/
Hiyo ndio asanti alipatiwa/
Kufanya nini/
Kuwatolea ma-idea za kuwasaidia/
Kuwabadilishia city/
Ukuta zote si ni through/
Ka mng'aro ya poko/
Ya ku-expose part ya juu ya mguu/
Ukiandika ma-assasinations
Ma-sniper maarufu/
Opposite building kwa roof/
Maiti zinaachwa kwa boot ya ndai/
Booth zinameza dough/
Time yako ya kuongea imeisha/
Adui wanakuwinda na harufu/
Kwa ile roho safi na moyo mkunjufu/
Ka Munyakei kuanzisha corruption zero tolerance/
Na kufungulia kesi ya Goldenberg alipewa asante gani/
Account iliarishwa design ya cholera/
Tushavumilia viboko chini ya ma-slave master/
Hadi kupigwa na mayai ya kuoza ka Kenyatta/