Van The DJ Kenya/Big Homie Van

Utamaduni wa Hip Hop tunaoupenda umesimama kwenye misingi na nguzo kadhaa. Moja ya nguzo hizi ni nguzo ya u DJ. Leo kwa mara ya kwanza hapa Micshariki Africa tumepata fursa ya kuweza kupiga gumzo na DJ aliyejikita kwenye muziki wa Hip Hop. DJ mwenyewe anatokea Nairobi, Kenya na anafahamika kama Van The DJ au kwa jina jingine Big Homie Van.

NB: Kama ungependa kuskiza Podcast ya gumzo hili badala ya kusoma nenda moja kwa moja hadi mwishoni mwa makala haya.

Van The DJ Kwenye Moja Na Mbili

Karibu sana Micshariki Africa kaka Van The DJ. Kwanza kabisa tuanze na wasifu wako Van unaitwaje, unatokea wapi na unajishughulisha na nini? Je umesoma nini na wapi na umefikia hadi wapi kimasomo?

Thanks for having me. Naitwa Van, Van The DJ in complete Van The DJ Kenya. Natoka Nairobi, na represent KE, Kenya au sio. Ninafanya shughuli kadhaa sana sana biashara kwanza halafu pia kuna events (matukio/matamasha) Mimi ni organizer na bado vendor (muuzaji) halafu pia kuna ku DJ, ku mix, ndio maana hapo kwa jina kuna hiyo The DJ.

Nilisomea IT halafu currently nafanya Sound engineering, niko halfway done.

Kwa nini unajiita Van The DJ au hata Big Hommie Van, haya majina yalikujaje na yana maana gani?

Jina Van ni nickname ilitoka kwa ma beshte wangu. Pioneer wa hili jina ni Amesh shout out kwake. Yeye ndio alinipatia hilo jina wa kwanza halafu Big Hommie pia imetoka kwa mabeste zangu eeh sana sana juu ya kile nafanya. Mi na play part ya kuwa Big Hommie kwa wasee kibao kama vile shughuli ya ku link wasee na opportunities (fursa). Mimi sio mtiaji ati kitu kikitokea, kama najua kuna form (mpango) mahali najiwekea, zi.

Mi huwa na link wasee na opportunities ama nasaidia hawa wasee place ninaweza ndio maana nikapata jina Big Hommie. Big Hommie ilitoka kwa ma hommie.

Van wewe ndio DJ wa kwanza sisi kufanya mahojiano naye. Kwanza kabisa tueleze kwa nini nguzo (element) ya DJ ni muhimu kwenye utamaduni wa Hip Hop. Pili DJ kazi yake ni nini?

Aah DJ ni important kwa sababu kwa Hip Hop DJ ana connect artist na crowd na pia analetea crowd vitu vipya ambayo hawajiskia before like ku wa introduce to dope shit hiyo ni kazi ya DJ ni very important kwa sababu sahii social media vitu kama hivyo vinajaribu kuleta hiyo break but unapata sanasana wasee hurudia ngoma kadhaa.

So unapata kuna monotony uki decide ku link na artist straight up ni fresh yes but kwa DJ kuna vibes like naweza nikakuchezea ngoma kadhaa zenye zinafanana na kuna a couple of them ambazo hutakuwa unajua so ni important sana especially sahizi kwa sababu sio kama kitambo kwani kuna media(vyombo vya habari), kuna hio connect ya straight artist kutoka kwa artist na crowd yake so ku intergrate wasee wote kama kuna Hip Hop heads mahali kujua like mimi nikihitaji kujua dope stuff (vitu vizuri) natoa wapi, hiyo ndo kazi ya DJ.

Alafu hiyo ya pili nilikua nasema hiyo bridge (kivuko) hata kama kuna social media na hizo site zote za ku stream, ku stream ngoma moja na kuskia hiyo mix ya ngoma kibao zimekua blended pamoja sio the same thing na haileti the same vibe

Wewe ulianzaje hadi kufikia kuwa DJ? Tueleze kidogo kuhusu historia yako ya nyuma ya kuwa DJ.

Nimekua nikicheza ngoma kwa miaka minane(8) kuanzia 2014 hadi sasa na bado tunaendelea na hiyo vibe. Nilikua nakaa na wasee ambao wanacheza ngoma kwa sababu nilikuwa napenda muziki toka utotoni. Kwa hiyo inapokuja kwenye muziki nimekua nikiiskia kwa mda sasa wakati ulipofika kuwa nataka kujifunza hii fani ilibidi nikutane na watu ambao wanafanya hiyo shughuli na nikafunzwa moja mbili.

Kwanza sikuanza na u DJ nilianza na turntablism ambayo ni ya kuonesha umahiri waku scratch na mambo kama hayo. Kisha taratibu nikaanza kua DJ kwa kila kitu na hapo ilikuwa ni mwaka 2014.

Van naona umejikita kwenye mziki wa Hip Hop. Kwa nini Hip Hop na sio mziki mwingine kama Lingala au Mugithi? Pia tueleze kuhusu hizo mixes zako za Hip Hop unazozifanya, nini kilikusukuma kuanza kuziandaa hizi mixes na kuweza kuwapatia mashabiki zako ili waweze kuziskia?

Nimekuwa shabiki wa muziki wa Hip Hop kwa mda mrefu sana na sikumbuki nikiskia aina nyingine za muziki kando na muziki ambao wazazi walikuwa wanacheza na kama ni mimi nachagua playlist nimekuwa nikiskia Hip Hop kwa mda mrefu sasa. Kwa hiyo ilipofika mda wa mimi kuanza kuwa DJ ilikuwa ina umuhimu sana mimi kucheza aina ya ngoma ambazo nimekua nikiskiza.

Halafu pia kitu kilifanya nianze kutengeneza mix za muziki wa Hip Hop ya Kenya ni kwa sababu kulikuwa kuna  na bado  kuna wasanii ambao hawatapigwa kwenye radio au unakuta ngoma yao huchezwa wakati wa kipindi cha muziki wa Hip Hop pekee. Yaani huwezi kaa ukaskia ngoma ya mwana Hip Hop ikichezwa kila wakati kwenye radio kwa hiyo nilitengeneza Kenyan Hip Hop Mix ilikuwa kwa ajili ya wana Hip Hop wenye uchu ya maudhui yetu na pengine haipatikani popote pale na kama ilikuwa inapatikana ni kwa eneo moja tu, umenipata?

Unapokuwa DJ unahitaji vitu gani ili uweze kufanya kazi zako?

Aaah kama ku mix kwanza nahitaji vitu kadhaa tu, sio vingi kama turn tables, aah mixer na laptop na yenyewe pia inatakiwa iwe na ngoma. Hapo nipo sawa, ngoma zitachezwa, ndio hivyo tu.

Changamoto unazozipitia kama DJ ni zipi?

Changamoto eeeh, challenges eeeh. Kusema kweli mimi sijui kama kuna challenges (changamoto), kwa sababu pengine nilipokua nikianza kulikuwa na changamoto ya kuwatangulizia watu kitu kipya ambacho hawajawahi kukiskia kwa hiyo kuwashawishi watu waskie kitu ambacho hawajawahi kuskia.

Ila kwa sasa hizo ishu ambazo watu wanaziita changamoto ndio vitu mimi huwa napenda kwa sababu hizi changamoto ndio zinatufanya sisi tutafute njia ya kuihepa au kuishi nayo. Yaani si vigumu kuweza kujua nini cha kufanya. Kama mtu ana akili ya mjasiriamali anaelewa hapa ndio pahala panapopatikana fursa kwani kama hakuna changamoto watu watafanya nini?

Kando na shughuli za kuwa DJ, nimeona wewe pia una podcast yako inaitwa The Syntax Era Podcast ambayo iliteuliwa pamoja na tovuti yetu Micshariki Africa kwenye tuzo za Unkut Hennessy Hip Hop Awards. Hebu tueleze kidogo kuhusu podcast hii, huwa mnaangazia maswala gani hapo?

Podcast inaitwa The Syntax Era Podcast ipo pale YouTube, iTunes, Apple Podcast, Google Podcast, Spotify yaani popote pale unaweza iskiza na kupata maswala tunayoyaongea.

Podcast yetu sana sana tunaongea juu ya Utamaduni na Sanaa na utamaduni wetu wa ki Africa na sanaa ambazo ni vile vinavyoendana pamoja. Ukishaingia kwa sanaa utakuta vile kuna watu wanajieleza kwa njia ya sanaa au sio. Kwa hiyo tunaongea juu ya vitu vinavyofanyika kila siku na tunajaribu kujifunza kutoka kwa matukio mbali mbali na pia kujifunza ili kuepuka na kurudia makosa yale yaliyotokea hapo mwanzoni. Hiyo ndio podcast yetu unaweza stream kwa majukwaa yote makuu, au sio?

Kwa mtu anayetaka kuanza kuwa DJ unamshauri afanye nini?

Hehehe, kama unataka kuanza kitu naweza kukwambia ni kwanza utafute kazi nyingine ya kufanya kwanza juu kama unataka kuanza inamaanisha haujaanza na unatakiwa ufahamu kuwa kila kitu unachojua kuhusu kuwa DJ sanasana inakuja na taarifa ambazo sio za kweli kwani ukija na ukaanza hiyo shughuli ya ku DJ utagundua kuwa haipo hivyo, ushanipata?

Kwa hiyo kama unadai kuanza ku DJ, chorea (lenga) na kama umeskia nimesema uchoree uka feel kuwa unataka kuilenga basi umefanya maamuzi sahihi. Ila sasa kama bado unataka kuifanya hehehe, hakikisha kuwa kinacho kuskuma ni hamasa kutoka moyoni yaani usiwe unatarajia watu wakukubali nje kwanza kwani utalemewa. Kwa hiyo hakikisha msukumo unaopata ni kutoka ndani hususan upande wa muziki na hiyo sanaa ya kupeleka kitu kwa watu na wakikubali, ushanipata?

Kazi zako unazipataje na gharama zako ni shilingi ngapi endapo mtu anataka kupata huduma yako?

Inategemea unataka kazi gani kwa sababu kama nilivyosema hapo awali tunaratibu matukio, tunauza bidhaa. Inategemea mahitaji yako na kwa malengo yepi kwani tunaweza ongea kisha tujue hesabu inakuaje kwani sina bei maalum inayoniwezesha mimi kusema bei yangu ni hii, zii.

Inategemea kile unachotaka na ukubwa wa kazi unaotakiwa kufanyika tutakuja na hesabu.

Je wewe mwenyewe ushawahi ku produce ngoma au kumuandikia mtu yoyote yule ngoma? Na je unapiga chombo chochote cha mziki?

Nasomea sound engineering sahii so niko na studio na nime record watu kadhaa ila mimi binafsi sio mdundishaji hivyo sijaunda mdundo wowote ambayo mtu anaweza tumia, hiyo ni ishu bado najifunza. Inapokuja kwa ala za muziki mimi nafinya finya piano nikimaanisha najua kupiga piano, yeah.

Unazungumziaje Hip Hop ya Africa Mashariki je ipo kwenye mwelekeo mzuri? Na je kando na Hip Hop mixes toka Kenya tutarajie mixes za mziki wa Hip Hop wa Africa Mashariki ki ujumla?

Ninafanya mixes za Hip Hop za Kenya hata hiki ndio kitu kimetufanya tumepatana sahii na kupiga hili gumzo. Binafsi naweza kusema vile niko na wasanii wengi wa Kenya niko na mahusiano ya ukaribu nao na ngoma ikitoka huwa wananitumia na nikitaka mdundo wa ngoma walioachia huwa napata hadi wakati nitakuwa na mahusiano ya ukaribu na wasanii kadhaa kutoka Tanzania ambayo kwa sasa wapo kadhaa ndio nasema mnaweza kuskia mix kutoka huko nje.

Kipi ambacho sijakuuliza ungependa kutuambia?

Binafsi napenda kusema haya maneno ninayoyasema kama unataka kuwa msanii kabisa hakikisha kabla hujaingia studio una mkakati, kwani kuingia studio sio mkakati hapo ushaanza kufanyia kazi mkakati wako.

Shukran sana kwa kukubali wito wetu na kuja Micshariki Africa. Tumejifunza sana kutoka kwako na natumai pia waskilizaji wetu na wasomaji wetu watapata kitu kutoka kwa hili gumzo letu. Nashkuru hadi hapo tutakapo kutana tena, asanteni!

Mcheki Big Homie Van kupitia mitandao ya kijamii

Faceboook: Ian Robert Ajow (Big Homie Van)
Instagram: vanthedeejay