Uchambuzi Wa Albam: Shadow Of Death
Msanii: Veryl Mkali Wao
Tarehe iliyotoka: 06.11.2021
Nyimbo: 15
Mtayarishaji Mtendaji: Level Next
Mchanganya Midundo Na Sauti: Edd The Beatsmith
Studio: 1183 Echochambers

Veryl Mkali Wao

Kwa emcee Verly Mkali Wao naweza sema 2021 umekuwa mwaka mzuri sana kwake. Emcee huyu mwaka huu amepiga kazi sana na juhudi zake zimeanza kuonekana. Veryl alianza kutuandaa kisaikolojia kwa ujio wake mwaka huu kwa kutupatia single yake Triggers akiwashirikisha Ash pamoja na TG, kisha akaachia No Gimmicks (singo ya pili ya mradi huu) na Hormonal Imbalance.

Pia emcee huyu alifanikisha kutoa single pamoja na kundi lake 1183 Da Underground (Level Next, Genetic Disorder, Veryl Mkali Wao), Nakuru High 5 Cypher pamoja na kupata mda kufanya challenge ya Khaligraph Jones ya Odinare Challenge. Ilipofika mwezi wa 11 mwaka huu Veryl akaona sasa mda ni mwafaka wa kuwabariki mashabiki zake mradi wake wa kwanza ambao ni albam kwa jina Shadow Of Death.

Binafsi mimi nimekua nikingojea mradi huu kama ujio wake wa pili na ulifika mda mwafaka. Mradi huu ambao umesimamiwa na kuundwa asilimia mia chini ya usimamizi wa producer Level Next haukuniangusha. Mradi wenyewe ambao ni boombap mwanzo mwisho umeundwa kwa umakini na kando na utunzi na uchaguzi wa midundo iliyotumika Veryl pia alikua makini kuchagua watu wenye uwezo flani ili wapige kazi pamoja.

Mradi huu ambao umebeba sahihi ya Level Next mwanzo mwisho una ngoma zilizosimama na kuvutia kibao kama vile True Love ambapo emcee huyu anaonesha vile mahusiano yake na mme wake Hip Hop ulipoanza kwenye mdundo mzuka sana wa LN. Pia kuna nyimbo kama Audio Biography ambao ni wimbo mzuka sana ambapo da’ Veryl anatupatia historia yake kuhusu alivyoanza kwenye hii tasnia ya Hip Hop na changamoto alizopitia hadi kufika alipofikia.

Nyimbo nyingine ambazo zinazidi kuonesha umahiri wa emcee huyu ni kama Enough is Enough akiwa na gwiji Romi Swahili, Vinare na Verdict ambapo wanashirikiana kuwaonya ma emcee gushi kua mda wao umefika tamati na lazima watoke jukwaani. Mdundo mzuka sana ambapo unapiga gita flani mzuka sana.

Emcee huyu pia haogopi kutufungulia moyo wake na kutueleza kuhusu maisha yake binafsi na maisha  yake ya mahusiano. Akiwa na Romi Swahili tena kwenye Blame Game wawili hawa waongelea maisha ya mapenzi ya kulaumiana. Wimbo mwingine mzuka sana wenye mada ya mahusiano ni Can’t Keep A Good Woman down akiwa na Sandra Solit. Sandra anabariki wimbo vizuri sana kwenye mdundo huu na ndio maana yupo kwenye nyimbo mbili kwenye mradi.

Gonjwa la msongo wa mawazo pia linagusiwa freshi kwenye wimbo mzuka sana Triggers (singo ya pili ya mradi huu) akiwa na Ash pamoja na T.G. ambapo emcee huyu anatupigia story kuhusu rafiki yake aliejaribu kujiua kutokana na changamoto alizokua akizipitia maishani mwake.

Kwenye Precious Love akiwashirikisha T.G. na Sandra Solit emcee Veryl anaongea na mboni ya jicho lake ambae na binti yake. Hapa anamwambia binti yake mazingira magumu aliyokuwepo wakati alipozaliwa. Wimbo mzuka sana ambapo unamtia moyo single parent yoyote. Kwenye kiitikio wageni waalikwa wanatendea haki mdundo wa LN.

Kwenye Shadow Of Death ambao ni wimbo unaobeba jina la albam da’ Veryl anatema nyongo kuhusu changamoto za emcee wa kike kufanikiwa kwenye hili game. Juu ya vinanda vya LN Veryl anasema,

“Ku make it kwa hii game ni tough as shit/
Believe me it only gets worse kaa wee ni chick/
Haijalisha what truth you speak how hard you spit/
Watasema we ni m-dope kama utaweza show your big ass na tits/
It makes me sick/
And to me this shows there is a lesson this whole thing teaches/
Ever wonder why kuna so many misters na not enough misses/
Ni because this industry haipendi queens inapenda bitches/
So kama we ni dame anza ku act ka whore na soon you are on your way to riches/
If not tafuta two lamps two genies ndio atleast upate more than three wishes/
Game iko designed for females to act vi sleazy/
To beat them at their own game maybe ukue Nazizi/
Staying true to yourself nani alisema ni easy/
Believe me kama we ni dame kwa hii game haikuwangi kitu rahisi/
That is why most of us tunaifanya for leisure/
Even though most of us this rap thing tunai treasure/…”

Mradi huu ni funga mwaka toka kwa emcee huyu ambaye ameweza kufanikisha ndoto yake ya kutupatia albam. Mradi huu una uzito ki maudhui, ki mashairi, ki midundo na pia kwa upande wa waalikwa walioshirikishwa humu. Japokua emcee Veryl amepitia changamoto kibao maishani mwake kwenye safari yake ya mziki ninachoweza sema ni kuwa tunashkuru kwa aliyopitia kwani ameweza kutupatia mradi ambao ameweka hisia zake binafsi. Mkali Wao kawasili.

Kupata nakala yako ya mradi huu wasiliana na Veryl Mkali Wao kupitia;

Facebook: Veryl Mkali Wao
Instagram: veryl_mkali_wao
Twitter: Veryl Mkali Wao

Au pia waweza kununua mradi huu kupitia tovuti hii

Website: www.verylmkaliwao.com