Wimbo: Dhamira
Toka kwa: Vichwa Vya Habari (Xp Experience & Nyenza Emcee)
Albam: Heshima by Abby MP
Tarehe iliyotoka: 24.10.2018
Mtayarishaji: Abby MP
Studio: Digg Down Records

XP Experience

Beti Ya Kwanza (XP Experience)

Dhamira ya Mungu amani na upendo, dhamira ya mwanadamu kuyatimiza malengo/
Dhamira ovu uchochezi uongo, nashangaa mwanadamu amezivuka hizo level/
Dhamira ni wazo lenye uasili, linalochochewa na nguvu ya roho fikra akili/
Linakuzwa kwa moyo wenye ujasiri, linalotetewa na kudhulumiwa kweye mwili/
Nitazidi kupaza kwa sauti hii, nikitayarisha agano la sasa la kutii/
Agano langu linafika kwa bidii ,fungua nyororo upate ujumbe wa unabii/
Amani na upendo vimeshakufa, hata nguzo ya umoja tayari ina nyingi nyufa/
Uzalendo ni maneno yenye sifa, kama umri ndo uzalendo maneno makubwa rika/
Tafakari kivipi utakuwa wewe, katika sanaa ya hip hop wengi ma mwewe/
Njoo karibu usikie na unielewe, dhamira imebadilika na sifa kubwa kiwewe/
Ulimwengu unachechemea sasa, dhamira ya walimwengu ni maovu na anasa/
Dhamira kuu mi nataka kuwa rasta, nile mboga mboga nyingi niweze kukwepa kansa/

Nyenza Emcee

Beti Ya Pili (Nyenza Emcee)

Kipo cha kumiminia ukichota, ukiamua kukimbia usihofie kuchoka/
Ubongo ndio njia unapo focus, dhamira isiwe ya kuingia na kutoka/
Zingatia unachotema mdomoni, jua tabia njema ni silaha ya mkononi/
Kinacho semwa hua hakitoki ndotoni, maana yataka moyo kuyasema ya moyoni/
Ndani sio nje acha fikra migando, kimbilio la nje hutokana na milango/
Makadirio ya kesho leo ndo chanzo, kua na matarajio kuendane na mipango/
Amali ina shaka na nikabu, usikubali haraka ile dhamira ya tabu/
Mbali na baraka za vibabu, tujali na kusaka maarifa ya vitabu/
Wenye umri mdogo tusonge wote, wenye mvi nyingi fursa msizikache/
Bora kua na pesa ndogo maisha yako yote, au kua na nyingi japo kwa mda mchache/
Ulivyo sasa ni vile ilivyo kua, fikra na matendo yako ya enzi hizo na unajua/
Dhamira ilivyo kama mbegu inakua, dhamira ikitumika ndivyo sivyo inaua/