Toka kwa: Vioxii Dedee x Kaa La Moto
Nyimbo: Alikufanya Nini?
Albam: Damu Na Wino
Tarehe iliyo toka: 21.11.2019
Muunda mdundo: Robatoz
Studio: Batoz Music Entertainment

Vesi ya Kwanza – Vioxii Dedee

Jamii ikamsifia sana mama ikamsahau na baba/
Mwenye nguzo na jitihada, ila bado akanyimwa shahada/
Sikatai upendo wa mama ni muhimu tena zaidi kwa familia/
Ila uwepo wa baba mwana uhitaji kukua kisaikolojia/
Ebu cheki, wanadidimia kwa lawama/
Walowadharau kina baba/
Maana wamelea wadada wenye mienendo ya vijibaba/
Watoto wa kiume kama mabinti, upungufu umekidhi wa usahihi kimaadili/
Malezi halisi ni akili ishia na kiki/
Fasihi ni uzazi, kuhimidi inabidi wawili/
Hakuna ndoa ama uhusiano duniani pasina dosari/
Fikiria mara mbili kabla kuwalisha wanao tofari/
Punguza kiburi mwana dada maisha mengi ya bahari/
Jihadhari ama utashushwa kila steji ya safari/
Wali tulikula kwa dagaa/
Maana kwa upwaa aligaaga/
Baada ya uzushi uliozua baba kuondoka bila kuaga/
Mapengo kisaikolojia isiyo zibikia ikatanda/
Ni swali isiyo na jibu nimejiulizaga mara kadhaa/

Vesi ya Pili – Kaa La Moto

Ni maandiko alimuumba Adam kabla ya Hawa/
Ni sawa na uwepo wa magonjwa kabla dawa/
Hawa ni bora kuliko Adam hiyo ni sawa/
Ila haimaanishi Adam hana ubora mbele ya Hawa/
Na pagawa nikiskia flani hatajiki/
Mbaya zaidi nikiskia dingi hathaminiki/
Hata waandishi wamechoka hawamwandiki/
Na wakiamua kumuandika wengi wana mdisi/
Neno baba nahisi kama linakosa maana/
Kwa maana wengi wanamkana wakimsifu mama/
Waungwa wanazozana yupi bora kuliko/
Yupi mzazi yupi mlezi yupi bora kwa mtoto/
Tuweke wazi kila mzazi ana hadhi kwa mtoto/
Bila baba sidhani mama angekua mja mzito/
Zile nyakati ana hustle toka jasho ili tule/
Lipa kodi leta msosi na usisahau ada ya shule/
Kila mama ni dhahabu ila baba ni shaba/
Aliniambia mama bila wewe angeishia ukahaba/
Kiukweli bila mama sijui labda angekaba/
Kwa kua mji wa Mombasa unashawishi kazi ya roba/
Mama nikimpa kumi wewe ntakupa tisa/
Si ungwana itokee sijakupa maksi kabisa/
Mama nikimpa camera wee nitakupa picha/
Akitokea ameipoteza wewe unapicha unaikumbuka/