Skiza Podcast Hii Hapa Au Mwishoni Mwa Makala Haya
Mwaka jana nilifanikiwa kuskia miradi ya wasanii Okysde (Deliver The Package: No Excuses) pamoja na Liquid Flow (Boy Wa Daggo) na hapa ndio nilipoanza kumfahamu mtayarishaji W4nj4u (inasomeka Wanjau) wa Glitch Records ambae alishiriki kwa utayarishaji wa miradi hii kwa namna moja au nyingine.
Niliamua kumtafuta mtayarishaji huyu ilitupige gumzo ili tuweze kumfahamu yeye binafsi pamoja na kazi zake za utayarishaji na mchango wake kwenye utamaduni wa Hip Hop nchini Kenya.
Karibu sana Micshariki Africa kaka Wanjau jukwaa la Hip Hop. Leo tumetimba Nairobi, Kenya ili kuweza kufanya maongezi na producer anae fahamika kama Wanjau. Kwanza kabisa tuanze kwa kufahamu kaka unaitwaje majina yako kamili
Thanks sana bro. Naitwa Joseph Wanjau, Joseph Wanjau Nguru.
Kaka Wanjau tungependa kufahamu unajishughulisha na nini?
Naeza sema mimi ni msanii in general lakini sana sana nimefocus na ku produce. Mimi ni producer wa Hip Hop but pia nafanya photography, nafanya kazi ya video, nafanya graphics. Niko kila mahali, jack of all trades.
Tueleze kidogo kuhusu historia yako ya muziki? Ulianzaje kazi za utayarishaji wa muziki?
Mi nimekua na interest na music toka nikue mdgo. Journey yangu ilianza vizuri high school. High school tulikua tunaroga na beshte wangu lakini hapo ndio nili realize nafaa, naweza kusaidia sana nikiwa producer ju hatukua na mtu mwenye anatu serve beats vile tulikua tunataka, mtu angetupea kitu tulikua tuna dai.
So ile time nimejikalia ku produce vi fiti nikaanza kua serious ilikua after campus, ile period unajiuliza haya unaenda kutafuta job ama msee anataka kuchukulia serious nikasema eeh wacha tu nikae tu chini nichukulie hii kitu vi serious inaweza ikani feed.
Tueleze kuhusu jina lako la kazi Wanjaau (W4nj4u), lina maana gani, lilikujaje na mbona ukaamua kuweka namba "4" badala ya herufi "A" kama njia ya kuwakilisha njia yako sana sana pale mitandaoni?
Jina langu ni jina langu in general, mi nilikaa chini nikaangalia sikua na hiyo interest yakutumia jina la lakabu juu nilikua naona hii ni mimi mbona nisi shine na jina langu ili nikijulikana isikue ile jina nilichagua alafu nijipate huko mbele najulikana na hili jina, lakini kidogo huko mbele najikuta sitaku kuhusiana na hilo jina, so nikaona wacha nitumie lile jina moja ninayo but sasa nikaamua hio 4 niiweke instead of A. Hiyo ilikua sana sana kwasababu ya social media, kwasababu niliona ukiweka jina lako moja kwa moja halitapita mara moja.
Hivyo nikajaribu Wanjau na 4 (alphanumeric/herufinamba) ikakukubali ndio nikaona si nitumie kama signature ya jina langu, ika weza.
Wewe una produce aina gani ya mziki?
Hip Hop na genre zingine on request. Ukiniambia nikufanyie kitu kama afro nitakufanyia.
Tueleze kidogo kuhusu miradi ambayo umeshaandaa pamoja na watu ambao ushafanya nao kazi?
Wale watu ambao nimepiga nao kazi ni kama akina Okysde, tulipiga DTP na yeye, Deliver The Package, nime work na Liquid (Flowz), tumepiga na yeye Boy Wa Daggo na Liquid bado tuko na kazi nyingine tumeshaandaa na yeye, imebaki kumalizia. Nimejishughulisha na Deniro, tumewekelea tracks kadhaa na tunafaa kuekelea projects na yeye, nani mwingine? Kuna boi mwingine mtaani mngori(mbaya) kutoka mtaani anaitwa Jeshi. Jeshi tulianza kuroga na yeye tukiwa high shool. Pia yeye ni kijana mwenye tumefanya kazi na yeye. Lakini hao ndio watu nimefanya kazi nao ile consistently.
Niileze kuhusu signature tune yako "Wanjau nichome". Ina maana gani na uliiundaje? Je ni muhimu na ni lazima kwa producer kua na signature tune au jingle yake?
Unaweze weke hiyo track kama inakuambia Wanjau nifanye niwe wa moto hivyo ndio naiona. Ni kitu ilikuja in the moment hivi. Ilikua kitu ya haraka, hata hiyo ni phone recording. Mwenye alikua ameirekodi hata alikua anatengeneze chipo (chips/kiepe) hivyo haikua kitu professional at all ila ilitokea vi fiti, ilinibamba, ilikua catchy.
Nadhani kidogo jingle ni muhimu kwasababu mimi personally najua kuna tracks nitaende kuskiza juu najua ni huyu producer ndio ametengeneza. Kaa ukiskia project kama Hit Boy ame produce hii project utakua eeh hata kaa ni msanii gani ila kwakua Hit Boy yuko pale lazima kazi itakua kali.
Naona producer pia inaweza ikasaidia sana for a fan kuweza ku identify kazi yake ju hakuna njia nyingine fan ataweza ku identify producer isipoa ni kuskia tag. So tag nimuhimu kidogo kwa yule producer mwenye anataka labda ku standout kwa ma fans wake, inasaidia.
Wakati unapotaka kufanya kazi na msanii, cha kwanza unachozingatia nini kabla hamjaanza kupiga kazi ?
Kabla nifanye kazi na msanii yaani mi hata siitishangi, yaani sitaki vitu mob. Mi nataka tu vibe iwe right. Yaani uwe yule msee tunaelewana, tunaheshimiana na tunaweze ku cooperate ju in the first place kitu tunatengeneza ni collaboration na hakuna vile tunaweza kutengeneza kitu fiti na energy zetu hazijakubaliana.
Tukiingia studio ni lazima tuwe tunaelewana, tunaweza ku vibe na tunajuana personally kidogo.
Je ma producer unaona kama mnapewa heshima yenu mnayostahili?
Generally hii industry sidhani kama inatuheshimu. Ukijuja kwa individuals ina depend ni nani una deal nay eye na huyo mtu pia ame kuzwaje na mzazi wake, juu nime deal na wasanii type mbili; kuna msanii mwenye atu treat ne heshima ataku treat vizuri, unajua. Huyu ni msanii mwenye yaani hiyo cooperation inafanya kazi itokee vi fiti.
Na bado kuna yule msanii mwenye roho yake iko kwa kukutumia na ku make the most out of you na ku use the least amount of energy. Unajua ile amekutumia hata hakuna ile kitu atakurudishia, hakuna kurudisha mkono nit u wee nitakunyanyasa aje.
Itaku shangaza sana ni kina nani wanatu treat vibaya ni watu hunge expect, watu umeheshimu kwenye hii industry ila wao hu treat producers kaa shiit.
Ma fans na feel ma fans generally wanatupea heshima. Na feel ma fans wengi nime meet wameni approach na heshima na unaona kidogo hata wako excited na kitu tuna fanya. Ma fans na feel ni love na respect mi shida ni kuna wasanii wenye vichwa zao ni bigi na hii industry pia haijui kutuheshimu.
Changamoto unazozipitia wewe binafsi kama producer ni zipi?
Ku maintain balance ya life na kazi. Kuna times unapata life ina demand more of you na unajua pia craft yako ndio I grow ikue na stand out pia lazima uipee time so hio pia ni challenge, lakini bado tunamiini tutaomoka(tutafanikiwa), hii ishu itajilipa.
Kama producer, unaongeleaje hali ya mziki Kenya? Je unakulipa kama producer au imebidi ujishughulisha na kazi zingine kando na mziki ili kuweza kujikimu?
Muziki yetu Kenya sahii hapa Kenya iko in a very interesting place, ina grow na inaanza kupata quality, imeanza kupata production value, tuko in an interesting place music wise sahii.
Ukicheza vi fiti na juu ya internet na feel unaweza ukatafuta njia yenye ukapata a stream of income from your music. Inaweza bidi pia ukawa na kazi nyingine on the side kujikimu for bills ndogo ndogo.
Unaongeleaje hali ya muziki Kenya? Kwasasa habari ya mjini ni Drill, kwanini hali imekua hivi?
Wakenya tunapenda kufuata wave hio ndio hukua kitu tume specialize kufanya na Drill ni wave kubwa sahii. Lakini pia unaweza ukasema tuko na wasanii ambao pia ni legit kwa side ya drill kwa mfano watu kama Buruklyn Boyz, niko na hommie wangu Danytox,, ana do drill fiti, Wakadinali but so far mi naona ni wave acha tuone kaa ita last.
I hope wataweza kupata njia ya kuifanya i evolve itawacha kuwa wave na labda utapata drill ime maintain hadi 2 -3 years down the line na hata more but for now me nitaiita wave but naona kuna watu wanaifanya vi fiti.
Mwaka 2021 ulikua busy sana kwako. 2022 tutarajie nini kutoka kwako bwana Wanjau?
2022 nataka kutengeneza kwanzo double the amount of projects ya projects ambazo nilikua nimetengeneza 2021 alafu nataka pia content yetu i grow na i mature i evolve ile yenye nataka wale wasanii nina work nao pia zile vitu zenye wanasema wanaongelelea vile wanaji package kuna venye nataka muziki yetu ikue ya actual good music vile unakaa chini ukiskia “Wanjau Nichome” unajua haitakua track ya kuchachisha tu, unajua si kuhusu sherehe tu.
This time najaribu kwenda for maturity sana kwa vitu tunatengeneza so pia hio itafanya kazi inaekelea ikue slow kidogo juu good music na good works ina take actual time kutengeneza na hiyo ndio kitu tunataka ku make this time. Good shit.
Ungependa kutoa ushauri gani kwa kijana yoyote anaye taka kua producer?
Dedication na consistency eventually ita work out which hata mimi mwenyewe naendeleanga tu tu nikijifunza. Production ni kitu yenye inahitaji time, pia ukiwa na kitu ka studio hio pia inatitaji doo/mkwanja sawia na vifaa pia.
Wewe hutumia vifaa gani ili kuandaa mziki? Je unapiga chombo chochote cha muziki?
Instrument yangu ni FL studio but iko kwa goals zangu ku learn keyboard huu mwaka like nataka kwanza ku learn more instruments ni kitu for sure it on add more kwangu.
Kipi cha mwisho ungependa kutuambia ambacho sijakuuliza?
Ningependa kusema I hope hii culture yetu itakuja ku realize how important it is ku support our producers ju venye sii hukua tume complain about our sound na venye Kenya hatuna hiyo beat ina stand out kama vile wa Naija wana stand out na sound yao au kama vile South Africa wana stand out na Amapiano ama Kwaito. Na feel wale watu wata change sauti yetu wata iboresha au watafanya tuweze feel proud tukisema hii ni yetu Kenyan authentic, haitakua hawa wasanii mnasema “support Kenyan artists” na mwenye ata change sound yetu kwa hii game ni producers na I hope culture yetu itakuja ku realize hivyo na waanze kutu support coz man huku tunapitia ka trash man. So I hope culture yetu itakua smart enough kutu support.
Shukran sana kaka Wanjau kwa kufika Micshariki Africa jukwaa la Hip Hop. Tumejifunza mengi kutoka kwako na najua waskilizaji na wasomaji wa makala zetu wamepata kitu kutoka kwako. Tunashkuru na tunakutakia kila la heri katika mishe mishe zako za utayarishaji.
Nashkuru man, kazi safi!
Mcheki Wanjau/W4nj4u kupitia;
Instagram: W4nj4u
Instagram: Glitch Records