Nyimbo: Ukubwa
Album: Ukubwa EP
Muunda mdundo: Jerry Mtata
Tarehe iliyo toka: 11.02.2021
VERSE 1 – Bad Ngundo
Umekua acha kulaumu/
Una majukumu/
Wakati haurudi nyuma utapoacha kujituma utapigwa munyu/
Tuliza kichwa kisha picha zoom/
Jiulize mwenyewe/
Ni nani ataacha yake afate yako akuhimize wewe/
Akutunzie familia, fatilia/
Kujipigania mwenyewe dhamiria/
Ukikata tamaa umekufa kifikra/
Na ukifata ujamaa ni fitna/
Pigania ugali wako/
Watoto waende chooni tuuone uhodari wako/
Ukubwa sio kufoka kwa madogo/
Ukubwa ni kusota kama dojo/
Sio ndevu, sio mwili, jumba/
Mtu mzima ni mwerevu, hii siri tunza/
Mtu mzima anatambua baada ya maisha ni kifo/
Na hapo ndipo, anagundua ibada nzito/
Itamfaa, itampeleka pema/
Hana maneno ya kinyaa, anabagua cha kusema/
Haongei kufurahisha genge/
Akiongea ni busara hana visa mbwembwe/
Mkubwa hana wenge/
VERSE 2 – Papaa Frege
Umeshakua sio/
Bila akili unaweza pigwa na haya maisha hadi ukajishisi kisusio,/
Hivo yaepuke matukio/
na ukumbuke kuwa tunaishi mara moja maisha hayana marudio/
So, ukubwa jina kataa/
Aliye gizani we mpe nuru sio unazima na taa/
Na pia shukuru we ukipewa sio unavimba kitaa/
Waombee dua sio kuwacheka wanaoshinda na njaa/
Na ukishajua, kuwa umekua, jua kuwa kifua/
Kinabeba siri nzito sio popote unatua/
Kata ukutane na magumu ndo tayari, ishakua/
Hakuna gumu la kudumu, ni kusali na dua/
Habari hii chukua/
Usifanye shida wimbo/
Wa mbele ndo huchelewesha foleni ila wa nyuma ndo hupigwa fimbo/
Braza we zama chimbo/
Madini chimba, umakini unahitajika zaidi ya jeshi kazini wakiwa lindo/
Najua unawaza salary/
Mishe zinaenda parallel/
Mambo yanakuvuruga kichwani hukumbuki hata tarehe/
Hatare, mentari hii ni habari kwa kina/
Ukishakua jua kuishi kwenye dhima/