We Need More Heroes! - Fivara

Kusema ukweli Simba (Diamond Platinumz) na A list artists wengine hawawezi kuupeleka muziki wa Bongo zaidi ya ulipofika. Tuwapongeze na kuwa acknowledge kwa juhudi zao lakini tutambue kwamba hakuna zaidi ya hapo.

Sijui kilitokea nini ila Kwevo alikuwa/bado yuko level sawa na baadhi ya giants wa Wapopo (Wa Nigeria) halafu kama akarudi tena nyuma. Anyways kama nilivyosema tuwapongeze, walipofika si haba panastahili pongezi.

Nini kifanyike sasa?

  1. Mara nyingi points zimekuwa ni zile zile kwamba "Wapopo" wana watu wengi diaspora na kwenye vitengo muhimu vya maamuzi. Inasemekana Wajuba wapo kwenye kila sekta duniani na unapoongelea watu aggressive kwenye kutafuta fursa lazima utawakuta. Lengo sio kuwasifia lakini ni muda sahihi wa kuandaa watu watakaotusaidia kutoka kwenye huu mkwamo. Hapa naongelea decision makers kwenye makampuni kama ya streaming, not necessarily decision makers lakini wawe watu ambao wanaweza wakaupush muziki wetu zaidi (hata kwenye playlists na kuandaa shows). I think hapa Uraia pacha (Dual Citizenship) nao ni muhimu sana.
  1. Ubunifu: Aisee hapa hata sitaki kusema mengi kwa sababu wote tunaelewa kwamba tumetoka kwenye kubuni kwa namna yetu tumeanza kubuni kwa namna ya wengine. Kama nilivyosema sisemi mengi hapa.
  1. Umoja: Wabongo tunajijua tulivyo hatupendani. Sisemi mengi hapa pia.
  1. Uwekezaji: Bado sanaa kwetu ni ridhaa yaani haijarasimishwa kuwa ajira rasmi kwa hiyo hata uwekezaji bado ni mdogo mno. Hii inaenda kwa serikali, makampuni, taasisi na watu binafsi, bado hela haziwekwi kusapoti vipaji.
  1. Ujanja ujanja mwingi: BASATA, COSOTA, Media, Wasanii, Wadau na Mashabiki hapa. Sisemi mengi wote tunajielewa Wabongo. Halali inaharamishwa na haramu inahalalishwa yani ili mradi tu. Hapa msisahau masuala ya show, mnajua kabisa tunavyozinguaga 😂
  1. Crab mentality: Roho mbaya, Chuki na Husda zinaturudisha nyuma sana Wabongo. Mwenye code anabaki nayo hataki kuwapa wengine. Sitoi mifano unaijua au katafute.
  1. Aggression: Tunawahi kuridhika pengine ni vitu tunavyopata havikuwa kwenye matarajio ndio maana unaona mtu akishafika level anaona baridi tu hapa pametosha.
  1. Seizing opportunities: Hapa ni kuwa na watu wanaoona fursa sasa na hii inaanza na wasanii wenyewe. How do you position yourself? Umeipata fursa unaitumiaje kuondoka?
  1. Strategizing: Mbinu muhimu kabisa hii, tutoke kwenye figisu za kifala twende kwenye figisu za maana. Ni kama kwenye uchawi tuache uchawi wa kurogana turoge tuchukue Kombe la dunia (I’m joking 🙃). Oya hayo ma show tunaona Burna sijui Wizkid kapiga hayatokei tu ni mipango na mikakati kweli sio mambo ya kuvaa macheni mpaka yanakuzidia uzito shingoni.
  1. Tunahitaji watu zaidi kwenye kiwanda cha muziki (professionalism): Kuna taaluma kwenye muziki wetu kiukweli bado hazipo na waliopo hawatoshi. Wengi tu mfano Managers (wenyewe kabisa wale sio mtu anaemfadhili msanii), A&Rs, Lobbyists, Marketers na wengine wengi bado hatuna. Watu wa muhimu kucheza kete muhimu bado hatuna. Ngoja niwape mfano kuna yule dada Seven Mosha au watu kama kina Sallam, kuna wale wanaandaa na kutafuta show nje ya nchi, People who can get our artists big collaborations.
    1. Support kwa new talents/fresh bloods in the game: Hawa wako energetic, wana mawazo mapya, wanajua dunia inaenda wapi. Wanaweza kutusaidia kuvuka kwenye huu mkwamo na siwatanii hapa nawapa kipaumbele rappers, wana potential ya kufika huko maana tunajua how knowledgeable rappers are basi tu kuna mambo yametokea kwa miaka kadhaa rap yetu ikarudi nyuma. Anyways new bloods, new talents wapewe kipaumbele.

Mambo ni mengi na mara nyingi yanajirudia kama mada ya kufua Twitter inavyojirudiaga. Pongezi kwa Kwevo na wenzie kwa walipofika ila it’s time sasa twende zaidi ya pale. Halafu hili suala sio kwenye muziki tu, hata kwenye soka na ubondia ni yale yale. Angalia alipofika Samatta au Mwakinyo, somebody has to go and take it zaidi ya walipofika. Tusiishie kuwa na hero mmoja kwenye hizi mbanga, we need more heroes.

    • Ni mimi mwandishi wako, Fivara/Magokoro.