Uchambuzi Wa Album: My Beautiful Song
Emcee: Wecky Flowz
Tarehe iliyotoka: 01.011.2021
Nyimbo: 9
Watayarishaji Watendaji: Tasla Beats, Biko Beats, Eddy K
Mixing & Mastering: Tasla Beats, Biko Beats
Studio: Rhodeway Records
Nyimbo Nilizozipenda: Intro, Maisha Ya Msanii, 944, Hammer & A Nail, Kwa Basement
Janga la Uviko lililoanza mnamo mwaka 2020 lilikuwa na athari kibao sana sio tu kiafya na kwa upande wa vifo bali hata kwa upande wa ubunifu inapokuja kwa wasanii wetu. Sijui ni mara ngapi mimi binafsi nimesoma na kuandika namna ugonjwa huu ulivyowaathiri wabunifu wetu sana sana wale waliotokea nchi zilizoweka utaratibu wa aidha lockdown ama curfew.
Ni kwenye mazingira haya magumu ambapo msanii ambaye alianza kama mshairi, Wecky Flowz naye akaamua kuchukua changamoto hii kama fursa na kuanza kuandaa mradi wake wa kwanza ambao ni album yake My Beautiful Song ambayo aliichia rasmi mwishoni mwa mwaka jana.
Mradi huu mzuri unafunguliwa na Intro akiwa na John Mo’re (Afrocentric) ambayo moja kwa moja emcee anaanza kufunguka kuhusu maana ya mradi huu pamoja na jina la album juu ya mdundo wenye bass mzuka na kiitikio kilichojaa hisia toka kwa John Mo’re. Anasema hivi kuhusu My Beautiful Song,
“I’d like to welcome you ladies and gentlemen to this session/
A member of my thoughts called My Beautiful Song/
I’ve been looking for solace at various places life experiences/
Have been making me feel like the nigga is worthless down and hopeless/
I stare at the mirror trying to find my old me/
But fuck it the look there is nothing familiar why the hell wouldn’t you all see/
My homies are thinking I’m out of my mind because I’m doing some poetry/
I tried to give some shorties my time but they took my life as a lottery/
Thinking of all my selfish decisions I’m having to struggle with my intuition/…”
Mradi unaanza rasmi na wimbo mzuka sana unaoongelea changamoto za maisha ya usanii kwenye wimbo uliotumia sampuli nzuri toka kwa Daudi Kabaka kutoka Kenya Musa. Kama vile mwanadada alivyoshindwa kuvumilia mateso ya mume wake Musa, Wecky Flowz anaongelea historia yake ya mziki na mambo aliyoyapitia kwenye mdundo wa Biko. Maisha Ya Msanii ni wimbo chanya sana.
Kutoka hapa emcee huyu anazama kwenye mapenzi kwenye wimbo ambao yeye akishirikiana na Liz Tino (Taji Mziki) wanaimba freshi sana kwenye kiitikio wakati akimpa mpenzi wake maneno yaliyojaa mahaba.
Mtayarishaji Tasla naye anachukua doria kwenye mdundo unaofuatia wa One Flow Freestyle ila ingekuwa bora kama ile “tag” ya Dreamlife ingetolewa kwani kujirudiarudia kwake naona ilikuwa sio nzuri. Ni wimbo wa mitindo huru ila umeundwa freshi tu.
Baada ya hapa tunaenda moja kwa moja hadi Hammer And A Nail ambapo amewashirikisha emcee Katapilla na muimbaji Kathy Kyalo (Taji Muzik). Kinanda kinapiga taratibu juu ya mdundo wa Boombap wakati ma emcee hawa wakichana na kukutahadharisha kuwa ukicheza nao watakumaliza (kiuchanaji) na kisha watakuweka kwenye jeneza na kulipiga misumari na kukuzika kwenye kaburi la sahau. Wecky Flowz kajitahidi kwenda mstari kwa mstari na mwalimu wake Katapilla.
Baada hapa emcee huyu anatukumbusha alipoanzia anapotupatia spoken word flani mzuka sana inaitwa Tedd’s Interlude akiwa na Thee Poet.
Kisha tunarudi kwenye ratiba zetu za kawaida kwenye Kwa Basement Pt. 1 akiwa na Venessah Sandra kwenye mdundo wa ki West Coast ulioundwa na Biko tena wenye bass wazimu sana. Kwenye wimbo huu emcee huyu anaongelea utafutaji wetu wa kila siku akitutia moyo kuwa hakuna kupumzika hadi ufike uliponuia
Wekesa Kanoga akiwa na I-xtra ni wimbo unaofuatia ambapo emcee Wecky anajigamba vile yeye amenoga (Wekesa Kanoga) kwenye wimbo flani wa majigambo ila umetulia akisema Wecky kuwa, “Mziki ni kazi na bado kipaji ndio maana tuna zoza…”
Uncut Cypher Vol.1 ndio wimbo unaotamatisha mradi huu. Kwenye wimbo huu amewashirikisha ma emcee Chumba (Afrocentric), Switch Manne na Liz Tino (Taji Mziki).
Emcee huyu katupatia mashairi yaliyokwenda shule, uwasilishaji nao ni wa hali ya juu kwani unaskia vizuri anachokichana. Inapokuja kwenye upande wa mada amegusia mambo kibao tunayoyapitia maishani mwetu na amefanikisha haya yote kwa kushirikiana vizuri na watayarishaji wake waliomchagulia midundo mizuri pamoja na wageni waalikwa kufanya kazi nzuri pia. Kupitia kazi hii tunaona vile janga la Uviko 19 lilikuwa ni fursa nzuri kwake kutuandalia wimbo toka moyoni My Beautiful Song.

Mcheki Wecky Flowz kupata nakala yako ya mradi huu kwa shilingi 500Kshs(Tshs 10,000.00). Pia mfuate kwenye kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii:
Facebook: Wecky Flowz
Instagram: Wecky Flowz