Toka kwa: WM (Misingi Nation)
Wimbo: Mwanao
Albam: Single
Tarehe iliyotoka: 15.11.2021
Studio: Kinasa Records

WG (Misingi Nation)

Beti Ya Kwanza

Unapowaza kifo anza kuthamini watu/
Kipo around take info wote tutakua wafu/
Mwanao hai nipo nipige angalau tafu/
Ukiniona nipe uzito kilo shavu so kavu/

Mwanao sina stamina nanyong'onyea kabwela/
Sijui lunch ama dinner I’m looser not winner/
No hela no usela dah! Connection sina/
Utaishia jela usifosi mega sima/

Mwanao ninasonga sina jikoo/
Sijui pumzi itakata kisa UVIKO/
Mateja wananyongaa, wanakiuka miko/
Mwanangu upo skonga, afiki hili andiko/

Soma kwa malengo, nafasi so ya nongo/
Kado kapata kitengo, hakuzitumia nondo/
Acha mawazo fyongo, nyumban hapa bongo/
Tuliumbwa kwa udongo, zitatu dissolve gongo/

Kiitikio

Tunakosa ukamilifu, ubinadamu nyingi kasoro/
Jimix usifeel sorrow, unaniskiza mwanao/
MWANAO/
Mwanao nakupa michoro ×2/

Beti Ya Pili

Zinapenya mpaka utosi, ideal vesi/
Yan hazmiss fosi, kama ideal gesi/
Vesi zina meta meta, skia nachokwambia/
Naona mnaleta leta, mazoea kuitana dear/

Matokeo huyaoni, love haiko reality/
Mapenzi ni electron, wave particle- duality/
Oya unazungukwa, kama cannot ceko/
Manzi unachuuzikaa, carrot keko?/

Eb mwanangu shtuka, yan kwenye giza toka/
Ushauri ulotukuka, mwanao nina foka/
Dunia utazunguka, usisahau ilikotoka/
Huzingui ukikumbuka,jinsi nyuma ulivyosota/

Jinsi gani ulivyohaso, kuitafuta kesho/
Mangapi ulonayo, yanofanya uwe spesho/
Huo ujinga ni wa kupita, usikupatie mateso/
Pinga pasipo kusita, mana utakutoa majasho/

Kiitikio

Tunakosa ukamilifu, ubinadamu nyingi kasoro/
Jimix usifeel sorrow, unaniskiza mwanao/
MWANAO! /
Mwanao nakupa michoro ×2/