Yohana Mwenda akiwa ofisini kwake.

Mwenda ni mchoraji ambaye kazi zake nilianza kuziona kwenye mtandao wa kijamii, Instagram. Michoro yake ilinionesha uwezo alionao kwani nilikutana na michoro iliyotumia wino pekee, michoro iliyotumia wino na rangi, michoro ya rangi, michoro ya vibonzo, michoro ya mijitu yenye sura za kutisha, michoro inayoonesha tamaduni mbalimbali, michoro ya wanadada warembo pamoja na michoro ya wanamziki wa Hip Hop.

Kama ujuavyo Micshariki tumejikita kwenye mziki wa Hip Hop kwanza hivyo moja kwa moja nilitafuta kazi zake zaidi zinazoenzi Hip Hop na kisha nikamtafuta yeye mwenyewe. Tulifanya mahojiano ya awali na kisha kufanya interview rasmi kwa ajili ya Micshariki Africa ambayo leo nina furaha kuwakaribisha muisome ili mumfahamu mwanasanaa huyu na sanaa yake pia.

Karibuni.

Karibu sana kaka Micshariki Africa. Kwanza kabisa naomba kufahamu jina lako?

Asante naitwa Yohana Mwenda maarufu kwa jina la Mwenda

Bio yako Instagram inakueleza hivi; illustration, comics artist, story board artist. Hebu tueleze hizi ni shughuli gani unazofanya?

Ni kweli hizi ni shughuli zinazohusiana na uchoraji. Illustrations ni michoro ya vitabuni yaani ni michoro ya kufundishia, comics ni hadithi za michoro na storyboard ni muongozo wa michoro utakaomsaidia camera man au director kuweka hadithi yake sawa sawa kwenye mtiririko wa film

Tueleze historia yako na sanaa yako, ulianzaje hadi kufika mahali ulipo sasa?

Sanaa nilianza nikiwa mdogo nilipoanza chekechea nilijikuta nikiwa napendelea kuchora picha za vitu mbalimbali hadi kufikia madarasa ya juu niliendelea kupenda sana kuchora na kuingia katika mashindano mengi ya uchoraji ya mashuleni na mengi nilikua nashika nafasi za juu lakini nilipomaliza masomo baadae nilianza kuchora katika magazeti ya IPP Media na baadae magazeti ya Global Publisher na jarida la Kingo ikiwemo Kingo Cartoon Strip inayochapwa Tanzania kwenye gazeti la Mwananchi pia Uganda, New Nision na Kenya pia Political Cartoon za website ya Kingo Magazine

Nimeona pia kwa baadhi ya picha zako kuna michoro ya wana Hip Hop kama vile Notorious B.I.G. Je wewe ni shabiki la mziki sa Hip Hop?

Yes mi ni mpenzi wa hip hop kabisa yaani kindakindaki

Je mziki husaidia ubunifu wako unapochora au ni kizuizi inapokuja kwa ubunifu? Pale unapochora unapendelea kuskiza mziki, na upi?

Yes kila muda nasikiliza hip hop music na huwa nazisikiliza kila ninapofanya kazi zangu za kiuchoraji napendelea zaidi hip hop music hasa old school.

Sanaa yako imepokelewa vipi na familia yako pamoja na jamii inayokuzunguka? Je unaona kama sanaa Tanzania inalipa na kukubaliwa Tanzania ?

Jamii yangu imepokea Sanaa yangu vyema kabisa na nimewafanya watu wengi watamani kuwa wachoraji off course sanaa inalipa na inapokelewa vizuri kabisa                      

Nini kifanyike ili sanaa iweze kukua Tanzania ?

Serikali iwekeze zaidi kwenye Sanaa ili iwe sehemu ya kupunguza tatizo la ajira kwani Sanaa ni kazi, Sanaa ni elimu na Sanaa ni burudani                                 

Nini changamoto na manufaa unazo zipata kwa kupitia sanaa yako?

Changamoto zipo hususan kwa upande wa vifaa vya uchoraji ni ghali sana pia upatikanaji wa vifaa hivi pia ni changamoto.

Kwa upande wa manufaa katika sanaa ni mengi kama vile kujenga mahusiano mazuri na watu mbalimbali lakini mwisho wa siku kipato kinapatikana cha kuendeshea maisha na kujikwamua na umasikini kama nilivyosema sanaa ni kazi nzuri sanaa ni elimu lakini pia ni burudani bila kusahau manufaa ya sanaa ni sehemu ya utamaduni.

Kando na Instagram una pengine art gallery yako ambayo mtu anaweza kufika na kuona kazi zako? Ushawahi kuweka kazi zako kwenye art exhibition yoyote ndani na nje ya Tanzania?

Bado sijaandaa page nyingine ila nina mpango wa kuandaa gallery ya mtandaoni  na kuwa na website nitakayokua nikiuza kazi zangu.            

Kazi gani uliwahi kuifanya unayojivunia sana kwa zote ambazo ushawahi kuchora?

Hakika kazi niliyowahi kuifanya ipo kwenye jarida la kingo                           

Kwa maoni yako unaona dhana gani isiyo kweli hujitokeza wakati watu wanaposkia wewe ni mwanasanaa au unafanya sanaa ?

Dhana inayosema kuwa msanii ni uhuni tu au kupoteza muda             

Teknologia imeleta manufaa gani kwako na kwa wana sanaa kiujumla?

Technology imesaidia sana kutuwezesha kufikisha Sanaa mikononi mwa watu kirahisi zaidi kuliko tulipotoka. Kwa mfano nikichora ujumbe fulani nikaupost baada ya dakika chache utafika kwa watu wengi ndani ya muda mfupi.                             

Wachoraji wapo wengi, ni nini unafanya tofauti na wachoraji wengine ili kuweza kuwa unique au wa kipekee?

Mimi napenda kuwa tofauti kwa kuchora mitindo mbalimbali ya michoro na natumia muda mwingi sana kujifunza wachoraji wengine wanachoraje na nafanya hivyo ili nibaki mimi yaani kuwa na michoro isiyofanana na wachoraji wengine        

Kando na uchoraji Mwenda anajihusisha na shughuli gani zingine?

Kwakweli sifanyi shughuli zingine zaidi ya sanaa kwa sasa          

Sanaa ni talanta au mtu anaweza kujifunza na akajua kuchora? Mtu akitaka kujifunza unamshauri aanzeje?

Unaweza kujifunza na ukajua ikiwa una kipaji husika cha uchoraji  mtu anayejifunza ni vyema akatafuta msanii mwenye uwezo na akajifunza au akapitia course zinazopatikana kwenye mitandao            

Kwa upande wa comics je umeshawahi kuunda character wako ambaye ungependa kumkuza awe na kufahamika kama vile akina Madenge?

Yes nina characters wengi ambao nikihitaji kuwandeleza inawezekana kulingana na hadithi na tabia zao                                         

Ni kipi cha mwisho ungependa kutuambia ambacho sijakuuliza ?

Cha mwisho watu na wadau mbalimbali wawaendeleze watoto wote walio na vipaji mbalimbali hususan Sanaa ya uchoraji wawape nafasi watumie vipaji katika kuyaendesha maisha yao Sanaa ni kazi Sanaa ni ajira Sanaa ni burudani na Sanaa ni elimu

Mashabiki wakitaka kuwasiliana nawe watakupata wapi?

Napatikana kwa page yangu ya

Instagram: mwenda_art
Au kwa njia ya
Simu/WhatsApp +255787268092

Shukran sana kaka Mwenda kwa kukubali kufanya mahojiano nasi.

Shukrani pia