Toka kwa: Zee Maya ft Jossian
Wimbo: Kioo
Albam: Single
Tarehe iliyo toka: 03.01.2019
Mtayarishaji: Dula Wetu
Beti Ya Kwanza
Haikufaa iwe sasa,sijamaliza pingili za huu muwa/
Na haitakaa iwe chafya ndio siri nitakayoamua/
Kwani umezificha namba,nisipime kiasi/
Kwa vile imekuja ghafla nashindwa nikubali basi/
Nilichotamani usiishe tuendelee/
Hatua ya kucheza mbali sikukubali initembelee/
Niambie upepo au umeguswa/
Nami sikumwaga nilipotoka,usisingizie utelezi umekuangusha/
Kioo, haijatosha jiunge niziangalie chunusi/
Kama nilikuwa nakosa usingerudisha matusi/
Sawa mi nilikutumia, hata nje ya kazi zako/
Nikamulika wapita njia, nicheke wakiumia macho/
Basi ungetoa sauti nje na yangu unipinge/
Sio ulivyokubali nyufa ili macho uyakinge/
Nikitoka usiku nikakutupe, kesho nitaamka peke yangu/
Na sitaki yanikute hautatangaza ya chumbani kwangu/
Kioo, amekuvunja nani/
Mi nataka nitoke mbona nikitazama sionekani/
Kioo, mi sio wa kwanza usinifunge/
Niruhusu nikuite tena ukiniitika nikuchunge..
Kiitikio
Ulitembea nilipochoka/
Kioo, kioo/
Nakuhitaji haijatosha,
Kioo, kioo usinipe/
Beti Ya Pili
Sio kuniomba nguo tu, haukuwahi kuniomba nizime taa nisijione/
Haukuwahi kuniomba niache niugue macho na nisipone/
Haukuwahi kuvimba kukataa/
Kiasi cha kuficha umbo lako, nikiacha kusifia nitakubali sawa ulinifaa/
Imeisha hali siwezi kuirudia/
Taahira akiokota miba njiani nyayo timamu zinamsujudia/
Sina we' tena mkononi/
Na nakuomba nitakaposinzia unitembelee ndotoni/
Napojiandaa kuchekwa najua/
Bila kiatu tope linauzaga soksi nipo njiani kununua/
Nipo njiani kuinua macho ya wengi mtaani/
Nitakapokatiza huku nimeifunga tai begani/
Unahisi mi sijajua, kwako nilikuwa tambazi/
Wakati ili unilinde mi niliacha mlango wazi/
Uliimba dansi nikakataa kucheza/
Bado ukanipa kicheko hata nilichotoa baada ya kupoteza/
Kioo,amekuvunja nani/
Mi' nataka nitoke mbona nikitazama sionekani/
Kioo, isiwe mwisho nakuhitaji/
Tangu umefahamu vya kwangu usiniache niitwe mkosaji/
Kiitikio
Ulitembea nilipochoka/
Kioo, kioo/
Nakuhitaji haijatosha/
Kioo, kioo usinipe/
Sitakuuliza ulichobeba/
Iwe kwa jua ama mawingu/
Ukiinama nitakupa bega/
Ibaki mchana au usiku/
Niambie nitakuona tena
Au nitumie mfano wa maji kusahau, sema/
Zee Maya