
259 Vol. 3
- Historia (Background)
“259 EP Vol. 3” imeanzia wapi kama wazo, na jina hilo lina maana gani kwako binafsi?
“259 EP Vol. 3” ni mwendelezo wa miradi yangu ninayo toa kwenye siku yangu ya kuzaliwa, tarehe 25 mwezi wa 9, mara nyingi ikiwa ni zawadi kwangu na kwa mashabiki zangu kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa. Baada ya kupata wazo la kutoa hii ya tatu kuna mabadiliko kwenye tarehe itakayotoka, yenyewe itatoka tarehe moja mwezi wa tisa lakini lengo haliko mbali sababu huo ndio mwezi wangu wa kuzaliwa.
Ni changamoto au tukio gani la kihistoria katika maisha yako lilichangia kuunda mradi wa EP hii?
Tukio la kihistoria lililochangia kuunda mradi wa EP hii ni kuondokewa kwa kaka yangu na baba mzazi. Baada ya msiba wa baba mwaka 2020 niliporudi rasmi kwenye muziki niliachia baadhi ya single na baada ya hapo ikafuata 259 EP mwaka 2021.
Kati ya nyimbo ulizoandika, ipi unaona ni kumbukumbu ya safari yako kama msanii?
“Ninachotaka” ni wimbo wenye kumbukumbu ya safari yangu kama msanii, humo ndani niliwaambia watu ninachotaka ni nini.
2. Kuhamasisha (Inspiration & Motivation)
Ni ujumbe gani ungependa mashabiki wachukue baada ya kusikiliza “259 EP Vol. 3”?
Haijalishi utapitia maumivu gani bado unaweza kusimama na kuendelea, bado unaweza kuyafurahia maisha maana nyakati hazidumu hubadilika badilika.
Ni nani au kitu gani kilikupa nguvu ya kukamilisha project hii, hata ulipopitia changamoto?
Msukumo wa kuendelea kutoa kazi zenye ubora ndio kitu kilichonisukuma kukamilisha mradi huu. Mashabiki na watu wanaonisapoti sanaa yangu waendelee kupata kazi nzuri.
Ungependa muziki huu uwaguse vipi vijana wanaopambana kufikia ndoto zao?
Muziki huu ningependa uwaguse vijana na kuwakumbusha kuwa wanapotafuta maisha wasisahau kuyaishi yani wapate muda wa kufurahia maisha. Kitu kingine nyakati za maumivu hupita tu kama zinavyoweza pita nyingine.

Fivara
- Kufundisha (Educational Angle)
Kuna funzo lolote maalum uliloliweka kimakusudi kwenye baadhi ya nyimbo za EP hii?
Ndio, funzo maalum nililoweka ni kuwakumbusha watu wanapokua wanafurahia nyakati nzuri wafurahie kwa tahadhari. Wasijisahau na kujisababishia madhara. Funzo lingine ni nyakati za maumivu huwa zinapita maana Wahenga walisema, “Baada ya dhiki faraja.”.
Ni ujuzi gani mpya uliojifunza katika mchakato wa kuandaa “259 EP Vol. 3” ambao ungependa wasanii wengine wajifunze?
Namna ya kuandaa wimbo wenye ubora, unaozingatia viwango lakini pia ubunifu kwenye kila wimbo maana kila wimbo una mada yake, energy yake, stori yake, mdundo wake — hivyo ni lazima kila wimbo ujibebe kiubunifu.
Unaona vipi nafasi ya muziki kama chombo cha elimu ya jamii katika kizazi cha sasa?
Muziki bado una nafasi kubwa ya kuendelea kuwa chombo cha elimu ya jamii katika kizazi hiki sababu ni ni chombo tofauti na vyombo vingine vya elimu… yani ni rahisi mtu kujifunza alichowekewa kwenye muziki kuliko darasani. Muziki unapendwa na kila mtu. Hauhitaji juhudi kuusikiliza hivyo kukiwa na elimu kwenye muziki watu watajifunza mengi.
4. Burudani (Entertainment)
Ni wimbo gani kwenye EP hii unaona utakua crowd favorite kwenye shows na kwa nini?
Wimbo wa “5 AM”, “Down”, “Hii Sio Freestyle 4” na “Who Do You Think?” naona zitakua ni nyimbo pendwa kwa mashabiki kwenye shows.
Uliandaa vipi nyimbo ili kuleta mchanganyiko wa hisia na vibe tofauti kwa wasikilizaji?
Nyimbo hizi zimeandaliwa sehemu tofauti na ndio maana zina vibe tofauti kwa kila moja. Zipo nyimbo zilizorekodiwa Mwanza na zipo zilizorekodiwa Arusha. Lakini pia hata watayarishaji waliotumika ni tofauti tofauti pia.
Kuna collaboration au production style yoyote ya kipekee iliyoleta msisimko zaidi kwenye kazi hii?
Yeah, watu wamenizoea mimi kama msanii wa Hip Hop naetumia sana beat za Boombap lakini humu ndani kuna versatility ya kutosha. Watu wakijipatia huu mradi ndio wataelewa nachosema ni nini.
5. Tamaduni (Culture)
Ni vipi “259 EP Vol. 3” inawakilisha utamaduni wako au historia ya mji/eneo lako?
Mradi huu unawakilisha jiji langu la Mwanza kwenye kibao kama “Hii Sio Freestyle 4” lakini unaonesha falsafa yangu ya kuendelea kupiga hatua na kuendeleza ninachokifanya.
Umechanganya vipi ladha za muziki wa kisasa na sauti za kitamaduni katika EP hii?
Nimechanganya vionjo vya asili kwenye Ep haswa kwenye wimbo wa “Hii Sio Freestyle 4” ambao una chants za kabila la Kisukuma kwenye sample iliyotumika.