Uchambuzi Wa EP: For The Record (The Intro)
Emcee: P-Tah
Tarehe iliyotoka: 08/12/2023
Nyimbo: 4
Midundo: Alex Vice, Aress 66
Mixing & Mastering: Aress 66
Studio: Big Beats Afriq, P-Mani Records
Nyimbo Nilizozipenda: Mtaani, Salvo 2, Kitu Sure
P-Tah yule msee wa ‘On My Case’ (OMC) amerudi tena na msururu wa EP mpya kwa jina ‘For The Record (Tha Intro)’. Kwenye mradi huu emcee huyu anazidi kuonesha ukuaji wa kipaji chake cha kuchana kwani kama wewe ni shabiki yake unakumbuka vizuri tu jamaa alianza kuchana mwaka 2020 wakati wa ma lockdown ya Uviko 19 kule Uingereza.
EP imesimamiwa na watayarishaji wawili tu ki midundo ambao ni Aress 66 pamoja na Alex Vice, wazoefu hawa kutoka kule 254.
‘Mtaani’ ndo ngoma inayotufungulia mradi. Kwenye ngoma hii mdundo alipita Aress 66 ilhali Igee anamsaidia P-Tah kueleza kuhusu maisha yao ya kila siku. Nimefurahi kuona hawa ma upcoming wawili wakipiga mboka pamoja kwani kila mmoja naona anazidi kukua freshi inapokuja kwenye maswala ya uandishi na uchanaji.
Kwenye kiitikio Igee anatuelezea kuwa unapotuona kitaa kinachotupeleka kule ni kusaka hela tu;
“Mtaani niko busy ju ya ganji/
Mtaani kama chizi niko hustling/
Kejani niko easy na jirani/
Hii ni life mtaani/
Mtaani niko busy I’m grinding/
Mtaani choche hizi mdagi/
Kejani usingizi hunipata/
Hii ni life mtaani/”
Nia ya kuingia mtaani iwe ya kuongeza maokoto sio tu kukaa vijiweni na kujenga maghorofa hewa.
Kwenye Salvo 2 bwana Tapi anajiita mchafua rada kwani amekuja kuchafua hali ya hewa. Kwenye ngoma hii emcee huyu anaongelea maswala yanayosibu kiwanda cha muziki. Kupitia ngoma hii jamaa anarusha risasi ya mashairi yake akilenga watu kadhaa kwenye kiwanda cha muziki kama vile wale wasanii wa Kenya walivyoamua ku diss Tanzania pamoja kutaja rappers kadhaa kama Khaligraph Jones, Elisha Elai, Breeder na wengine wengi! 'Salvo 2' ni muendelezo wa 'Salvo' kutoka kwa EP yake On My Case 2
Pia anaongelea wasanii kuzidi kuunda muziki mzuri,kujiandaa freshi kwa ajili ya matamasha pamoja na kuhakikisha wanapiga promo ya muziki wao pamoja umuhimu wa kuwalipa pamoja na kuwapa maua yao watayarishaji wetu wanao fanya kazi nzuri.
Na pia sisi ma blogger tumeguswa na kuambiwa tufanye kazi nzuri, umuhimu wa kuwekeza tunachokipata kwenye sanaa yetu. Mashabiki wa muziki pia kuna neno lenu kule.
Mdundo mzuri kutoka Alex Vice.
'Ndio Hii' ambapo yumo Aress 66 kwenye mdundo unamkuta jamaa akipiga nondo za majigambo kuonesha kuwa naye yupo vizuri kwenye Mic akichana kama vile anapumua, pia kuna subliminal ya Octo hapa.
'Kitu Sure' wanashirikishwa ma emcee Brima Maoeve na gwiji Kitu Sewer. Kwenye mdundo flani unaopiga mdogo mdogo. Baada ya P-Tah kutema beti zake mbili za kufikirisha zikilainishwa na kiitikio kutoka kwa Brima Kitu Sewer anafunga wimbo akitukumbushia pia “Sii wote tungekuwa Uni nani angekuwa unique?” kitu sure hicho.
Kwa mawasiliano mcheki P-Tah kupitia
Facebook: P-Tah Wa Furu
Instagram: @p_tah
Twitter: @pmanirecords1